About YESU NI MUNGU
1. THIBITISHO LA KWANZA
Ufunuo wa Yohana 1:8 Yesu akasema, "Mimi ni Alpha na Omega, mwanzo na mwisho, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja Mwenyezi."
Ufunuo wa Yohana 1:17-18 "...mimi ni wa kwanza, na wa mwisho, na aliye hai nami nilikuwa nimekufa; ...na tazama, ni hai hata milele na milele."
Yesu alisema yeye ndiye wa kwanza na wa mwisho, hakika hili lamthibitisha yeye ni Mungu, kwa maana Mungu wa Israeli alisema katika kitabu cha Nabii Isaia 44:6 "...Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu."
Je, ni thibitisho lingine lipi tunahitaji litufahamishe Yesu ni Mungu?
Kuelewa jambo hili vizuri utapaswa uelewe hali mbili za asili ya Mungu (dual nature). Mungu ambaye ni Roho alichukua mwili wa nyama kwa muda wa miaka thelathini na nusu "Emmanuel".
Yohana 1:1 "Hapo mwanzo kulikuwako na Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu."
Yohana 1:14 "...Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu ---" (Mungu) alifanya jambo hili aweze kutoa uhai wake na kumwaga damu kwa ondoleo la dhambi zetu.
2. THIBITISHO LA PILI
Yohana 4:2 "...Na mara nalikuwa katika roho, na tazama kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na Mmoja ameketi juu ya kile kiti."
Ufunuo 4:6-8-- "Na kwa kile kiti kulikuwa na makundi yaliokuwa yakimwabudu aliyekalia kiti hicho."
Mstari wa 8, unatuelezea vizuri ni nani aliyekuwa amekikalia kiti hicho. "Wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu Bwana Mungu mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.
Ufunuo 1:8 Yesu akasema ya kwamba yeye ndiye aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja, Mungu mwenyenzi. Kuna Mungu Mwenyenzi mmoja tu.
Ufunuo 4:11 "Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote,--"
Yohana 1:3 na (10)... yazungumza juu ya Yesu ya kwamba vitu vyote viliumbwa naye, na ulimwengu haukumwelewa.
Wakolosai 1:16-17 Mtume Paulo alisema,"kwa kuwa katika vitu vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake," Na kwa thibitisho zaidi ya kuwa Yesu Kristo ndiye Bwana Mungu Mwenyezi, tunasoma kwenye kitabu cha Isaya 44:24... Mungu mwenyenzi kwa agano la kale akisema..."Mimi ni Bwana, nifanyaye vitu vyote, nizitandaye mbingu peke yangu; nienezaye nchi; ni nani aliyekuwa pamoja nami;
Ufunuo 5:9.... Nao waimba wimbo mpya kwa Mwana kondoo wakisema, "Wewe ....ulitukomboa ukamnunulia Mungu kwa damu yako..." Damu ya nani?
Show more